NI Mshindi wa tuzo ya muigizaji bora wa kike 2015, Irene Paul ameandaa filamu kama zawadi kwa mashabiki wa filamu kwa kutambua kazi anazozifanya na kumpigia kura nyingi zilizompa ushindi.
Akizungumza na Gazeti la Nipashe Irene alisema ana washukuru Watanzania kwa kumpokea tangu alipoingia katika uigizaji lakini pia ameamua kutenfgeneza filamu ambayo bado hajaipa jina ikiwa ni kwaajili ya kurudisha hisani kwa wanaomkubali.
Irene ambaye alishinda tuzo hiyo ya muigizaji bora wa kike kupitia filamu ya Never Give Up alisema amegundua Watanzania hawapendi waigizaji wanaofanya kazi kwa mnazoea.
>>>Kwa kweli bila mashabiki wa filamu mimi nisinge kuwa bora,<<alisema
“Napenda kusema naandaa filamu mpya kwa ajili ya shukurani kwa Watanzania amabo ndio mashabiki wetu.
0 comments:
Post a Comment