daaaah!! jamani kila jamii ina tamaduni zao katika ulaji wa vyakula na kuna nchi za wenzetu ulaji wa nyama ya mbwa, panya, sungula si kitu kigeni kwao na hutumia kama kitoweo kila siku lakini kwa wengine huona ni jambo la ajabu na haramu kwao kutumia.
Kuna stori kutoka Nigeria kwenye mji wa Anambra ambapo Mgawaha mmoja umedaiwa kuwauzia wateja wao nyama za binadamu tena kwa bei kubwa tofauti na bei nyingine.
Inasemekana Polisi walipewa taarifa hizo na kuamua kufanya uchunguzi na ndipo walipovamia mgahawa huo na kukuta vichwa viwili vya binadamu vikiwa ndani ya mfuko na tayari vimekatwa. ama kweli dunia inapoelekea siko
0 comments:
Post a Comment