+10 344 123 64 77

Sunday, May 10, 2015

MAZOEZI KWA WALE WENYE MATUMBO MAKUBWA NA WANAOTAKA KUWA NA 6 PART===>>soma hapa

Ndugu zangu leo nataka kuelezea baadhi ya mazoezi ambayo yatakusaidia kukata Tumbo lako vizuri kama yatafanywa vema,ila kaa ukijua kwamba mazoezi haya pekee hayawezi kukupa matokeo mazuri kama hutashiriki mazoezi mengine ya kupunguza mafuta kama kukimbia,kuendesha baiskeli,kuogelea,kutembea haraka haraka,kucheza mpira na mengine mengi soma topic iliyopita,Mazoezi haya ni kwa ajili yakutengeneza masozi(muscles) za tumbo kuwa ngumu na kukupa shape nzuri(six packs),hata kama yanakata mafuta basi ni kwa asilimia ndogo sana kwahiyo usifanye haya mazoezi peke yake ukidhani kuwa ndio utapunguza tumbo hapana.

ONYO
Mazoezi ya tumbo ntakayoyaelezea yafanywe kwa umakini sana kwa watu ambao walisha wahi kufanyiwa upasuaji wowote wa tumbo ikiwa ni wanawake kwa uzazi au kwa matatizo mengine yoyote,kwani yanaweza kukuletea matatizo mengine makubwa zaidi.

Tumbo kama tumbo limegawanyika katika sehemu mbili:Tumbo la juu na Tumbo la chini,Katika mgawanyo huu kila sehemu ya tumbo inamazoezi yake ingawa yapo yale general kwa ajili ya tumbo zima.





  • Lala na mgongo kama tulivyoona zoezi la kwanza ila hili tofauti yake sasa badala ya kukunja miguu unakuwa umeinyoosha kama kawaida ila sasa wakati unanyanyua sehemu ya juu ya mwili unakunja na mguu mmoja kuufwata huku mwingine ukiwa umenyooka,mfano wake ni kama mtu ukiwa unaendesha baskeli unavyokunja miguu kwa kupishana,Rudia mara zile zile kama nilivyoeleza kwenye zoezi la kwanza. Angalia mfano huu...

  • Rudia kulala na mgongo miguu yako kunja kama tulivyofanya zoezi la kwanza ila sasa hili tofauti yake ni kwamba badala ya kunyanyua sehemu ya juu kidogo na kugeuka upande mmoja baada ya mwingine,hili una nyanyua sehemu ya juu ya mwili na kufwata magoti yako moja kwa moja,kwa wanao anza hili ni zoezi gumu kidogo inabidi uwe na mtu akushike miguu ili uweze kufanikiwa kulifanya au kama unamahali unaweza kuchomeka miguu ili kujizuia,lugha ya kigeni tunaita (Sit ups on floor) angalia mfano huu...

  • Zoezi hili pia unaweza kulifanya kama una bench lako zuri kwa ajili ya mazoezi ya tumbo au kama uko GYM zoezi hili ni zuri sana kama utaweza kulifanya kwani linagusa karibu matumbo yote la juu na lachini,kumbuka kufanya kwa round tatu na round moja fanya mara 7 na ukipumzika sio zaidi ya dakika moja kwa mara moja.angalia mfano...

2.Mazoezi ya tumbo la Chini:
Hili ndilo tumbo gumu kutoka kuliko maelezo na limekuwa likisumbua watu wengi sana,lakini ukilizingatia kwa mazoezi magumu kidogo kwani hakuna kitu kizuri kiraisi lazima usote kidogo linakwisha na utabaki na umbile lako zuri kama kawaida,(work hard for better Achievements)
  • Kama kawaida lala na mgongo na miguu yako yote uwe umenyoosha,mikono yako iwe nyuma ya makalio yako then nyanyua miguu yako nyuzi 90 na kuirudisha chini tena fanya hivyo kwa mara 7 na kupumzika sekunde chache na kurudia hivyo kwa mara tatu. hili ni zoezi zuri sana kwa tumbo utalisikia mapema

0 comments:

Post a Comment