NI Alhamisi ya May 21 2015 kwenye story za kiburudani kwenye XXL AT Cl0udsFM, Abidad anakuwa mtu wa kwanza kukaa kwenye headlines.
Jamaa amesema kabla ya kufanya kazi na Ali Kiba alihangaika sana kumtafuta, kila wakienda kwao kule Kariakoo wanaambiwa Kiba hayupo, baadae alifanikiwa kukutana nae na akampa CD yenye beat.. mwisho wakafanikiwa kufanya kazi.
Mastaa wanabania undergrounds? Nay kathibitisha kwamba hiyo sio kweli,Nay na Mr. T Touch wameamua kufungua milango kwa wasanii wanaochipukia kwenye muziki ambapo hao waliopata nafasi kazi inaanza kufanyika Studio ya Free Nation Records chini ya usimamizi wa mkali mwenyewe t touch.
May 21 ni siku ya kumbukumbu kwa ndugu zetu waliofariki katika ajali ya meli ya MV Bukoba mwaka 1996, mwanamitindo Flaviana Matata ni mmoja ya watu ambao walipoteza watu wao wa karibu kwenye ajali hiyo.
ni Flaviana alimpoteza mama yake mzazi kwenye ajali hiyo, leo yuko Mwanza kwa ajili ya kufanya ibada ya kumbukumbu ya ajali hiyo.. Flaviana amesema ni vizuri viongozi wakaipa umuhimu kumbukumbu ya siku hii ya leo kwa kuwa ni watu wengi waliopoteza ndugu zao kwenye ajali hiyo.
0 comments:
Post a Comment