+10 344 123 64 77

Saturday, May 16, 2015

STIVEN KANUMBA( THE GREAT):: AREKODI SINEMA INAYOAKISI MAISHA YAKE====>>angalia hapa

Aliyekuwa mwigizaji nguli wa filamu za bongo movies, Marehemu Steven Charles Kanumba "Kanumba" enzi za uhai wake.
====>>WIKI iliyopita tuliishia pale Kanumba alipoanzisha uhusiano na mwigizaji ambaye wakati huo alikuwa kinda wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’. Uhusiano wao ulikuwa wa siri sana na watu wengi waliubaini pale Kanumba alipofariki.
ENDELEA...ZAIDI HAPA CHINI
Mbali na kufanya vizuri katika anga la filamu, Kanumba aliweza kutoa michango mbalimbali katika jamii. Katika michango hiyo, aliweza kupewa ubalozi mbalimbali kutoka katika makampuni yaliyotambua mchango wake.
Akatajwa kama Balozi wa Oxfam. Oxfam ni kampuni ya Waingereza ambayo ilianzishwa mwaka 1942 ambayo ilikuwa ikisaidia nchi ambazo hazijakomaa kiuchumi kama Tz.
Kama hiyo haitoshi, Kanumba alipata ubalozi wa kampuni ya StaR Times. Akatunukiwa simu ya BlAckberry na Kampuni ya ZAntel kwa kazi nzuri ya filamu aliyokuwa anafanya.

0 comments:

Post a Comment