NI UKWELI USIOPINGIKA Ukitaka kuchukiwa Duniani we KUWA MKWELI TU!!! kuwa mkweli kwa rafiki zako, kuwa mkweli kwa ndugu zako kuwa mkweli kwa wanaokuzunguka kuwa mkweli kwa jamii... mtu akikukosea mwambie kiroho safi, kitu kikikuuma ongea, kama kitu hujapenda ongea.. unaona shogaako akichemsha kitu mchane na kumuelekeza.. nk utachukiwa mpaka basi na utapewa maneno kama kimbelembele, mjuaji, mi sikipendi, ye ananjifanya hakosei
Na ukitaka kupendwa na kila mtu Duniani na wengi wawe wako we SNITCH TU.. njia ya kufanya ni KUSNITCH TU... mtu akikosea weka bonge la kinyongo halafu akipita mbele mtolee tabasamu paaana la plastiki, rafiki yako akichemka kaa pembeni mtete hatari akitokea mbele yako mwambie bravo we jembe umewakomesha n.k, kitu kikikuumiza teketea nacho rohoni tu usiongee wala nini halafu mbele yao unawaonesha hawajakosea huku unatafuta njia ya kuwakomesha na wao kichinichini, mtu akikuboa hata kama rafiki yako mchekee tu akigeuka mpe bonge moja la sonyoo... hapo utapendwa na Dunia nzima.. na we ndio utakuwa mzuri kwao bila kujali VINYONGO MIA NANE ulivyovibeba juu yao... na huyu kimbelembele mtoa dukuduku atapewa majina yote...
Tunachosahau hata msema kweli haongei ukweli kwasababu yeye yuko PERFECT...hapana!!! ama hakwambii ili wewe usimwambie.. hapana.. hata yeye anahitaji kuambiwa na kuelekezwa km anavyofanya kwako lakini kosa ni la kwako kushindwa kumuelekeza na yeye anapokosea na kulibeba rohoni wakati huenda mwenzio alivyoongea ndio yameisha palepale.. wengi tuliowakumbatia SIO WAZURI KWETU ila tunawabeba sababu wanatuambia vile TUNAVYOPENDA KUVISIKIA.
By Zamaradi Mtetema 0n Instagram
0 comments:
Post a Comment