Juma Ally akionyesha jeraha alilolipata baada ya kumwagiwa maji ya moto na mpenzi wake.
Na Haruni SanchawaMAPENZI kiboko! Juma Ally, mkazi wa Mongolandege Ilala jijini Dar es Salaam, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kumwagiwa maji ya moto na mpenzi wake, Swaumu Shemsanga, kisa kikidaiwa kupishana kauli kwenye mazungumzo yao
maji ya moto Juma Ally.
Chanzo makini kimelieleza gazeti hili kuwa tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Juma kwenda kwa rafiki yake huyo na katika mazungumzo hayo, kudaiwa kuwa mwanaume alimwambia mpenziwe kuwa huo ndiyo umekuwa mwisho wa mapenzi yao.
Inadaiwa kuwa baada ya kauli hiyo, mwanamke huyo alimmwagia maji ya moto mpenzi wake, ambayo wakati wa mabishano alikuwa akiyachemsha.
0 comments:
Post a Comment