NI Picha iliyosambaa mtandaoni ya Staa wa Bongo Movie,Wema Sepetu akiwa na aliyekuwa mchumba wa msanii wa Bongo Fleva,Linnah Sanga aitwaye Naga imezua utata baada ya mashabiki wa mwigizaji huyo kuhisi huenda amejiweka kwa mwanaume huyo baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Staa wa Bongo Fleva,Diamond Platinumz.
Taarifa kutoka ‘kitaani’zinasema kuwa wawili hao wameingia kwenye uhusiano wa kimapenzi ili kulipiza kisasi cha miaka kadhaa iliyopita baada ya kusemekana kuwa Linnah aliwahi ‘kutembea’ na msanii Diamond.
Hata hivyo Linnah akizungumzia ishu hiyo alipokuwa akiongea kupitia Uheard na Soudy Brown alisema kuwa alishaachana na mpenzi wake huyo miezi miwili iliyopita na kwasasa kila mtu ana maisha yake kwahiyo hajui kama kuna uhusiano unaoendelea kati ya Wema na Naga.
‘Mie nishaachana na Naga miezi miwili iliyopita nipo na maisha yangu kwahiyo sijui kama Wema ana uhusiano wa kimapenzi na Naga,’alisema Linnah.
Msanii Diamond naye alipoulizwa kama alishawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Linnah alisema kuwa hajawahi kuwa naye kimapenzi.
0 comments:
Post a Comment