Ni meibua wasanii wengi ila wasio na shukrani wachache, wengine wanakubali na kunishukuru popote wanapoulizwa, nami natanguliza shukrani zangu za dhati na Mungu atawabariki na mtafika mbali zaidi.
Wengine walikuja mikono nyuma na kunipigia magoti kuomba niwaingize kwenye filam na nikafanya hivyo huku wakilalamika wakina fulani wakiwaomba misaada wanawatukana na mimi ndiyo kimbilio lao, kwa kuwasaidia sikujali sura zao nzuri au mbaya, lakini leo wanawapa credit hao hao waliowatukana mwanzo kwa kuwaibua, lakini nasema tu huo ni ulimbukeni wao na ushamba wao na kutokuwa na sura ya haya wala nafsi kuwasuta.
Wengi tunapokuwa nashida ni wakwanza kumkimbilia Mungu kwa kuomba msaada lakini Mungu anapotupa msaada tunaoutaka tunamsahau na kumkimbilia shetani na mambo yake, lakini mzazi anapokuzaa hata akikupiga wewe bado utasema huyo ni mzazi wako.
Ila nafsini mwao wataendelea kunishukuru hata kama wanashindwa kushukuru mbele ya watu.
Hapa ndipo ule msemo wa 'tenda wema nenda zako usingoje shukrani' unahusika. Usife moyo Lucy Mungu atakulipa na uendelee na moyo wa kuwatoa wengine zaidi.
0 comments:
Post a Comment