Ni neema nyingine kwa Diamond na Vanessa Mdee baada ya kutajwa kuwania tuzo za MTV MAMA za nchini Africa Kusini zinazotarajiwa kufanyika leo usiku huko Durban, Afrika Kusini, hivi karibuni wasanii wametajwa tena kuwania tuzo zinazojulikana kama African Entertainment Awards (AEA) za nchini Marekani.
Kwenye tuzo hizo za African Entertainment, Diamond Platnumz ametajwa katika vipengele viwili ikiwa ni kipengele cha Hottest Male single of the Year na wimbo wake wa ‘Ntampata wapi’ unaoshindana na wimbo wa Aye wa Davido, Originally wa Fally Ipupa, Get Low wa DellonFrancis na Lobiwa R2bees.
Kipengele kingine anachowania Diamond ni cha Best Male Artist of the Year akishindana na Fally Ipupa, eddy Kenzo, Wizkid na Sarkodie
0 comments:
Post a Comment