+10 344 123 64 77

Friday, July 17, 2015

NIMETENDWA HAYA NA MDOGO WANGU MWENYEWE.......... YAPI HAYO?? SOMA ZAIDI HAPA CHINI====>> UJUE STORI NZIMA

MIMI ni mwanamke mwenye umri wa miaka 24 nna umbo zuri watu wananisifia kila napopita, kuhusu elimu nimehitimu chuo mwaka juzi.. Mimi kwakweli mpaka sasa naumia nafsi kila nikikumbuka alichonitendea mdogo wangu.

Kwani ni mdogo wangu wa damu kabisa na nilimuamini kwa kila kitu yani sikuwahi kufikiri kwamba siku moja atanitenda, Jina langu naitwa Nancy nimezaliwa katika familia ya
watoto sita wakiume wanne wakike tupo wawili Nyumbani ni arusha kabila ni mmeru.

Nimeamuwa kumsimulia mwandishi wa tovuti hii yamasainyotambofu.com na hii jamani ni Stori ya kweli naombeni ushauri kwa yeyote atakaeguswa na mkasa huu, Katika pitapita za kimapenzi nilifanikiwa kukutana na mvulana Fundi Computer mitaa ya posta jijini dar wakati nikiwa masomoni IFM, Bwana huyo alifahamika kwa jina la 'Deju', Deju alikuwa mwanaume mtiifu na mwenye kunijali nitake nini asininunulie?.. Kila nilichotaka alininunulia labda vilivyo nje ya uwezo wake tu ndio alishindwa kuninunulia.

Nilimtambulisha kwa marafiki zangu wote na ndugu wote maana mara nyingi wakati wa likizo tulifunga safari kuelekea nyumbani kwetu Arusha kuwasalimia ndugu zangu, Dar Es Salaam nilikua naishi kigamboni kwa mamkubwa na baada ya hapo niliamua kupanga chumba ambacho nilisaidiwa kulipa kodi na mpenzi wangu ili tuwe huru katika mapezi yetu, Ila cha ajabu yeye hakuwahi kunipeleka kwao wala kunitambulisha kwa mmoja kati ya nduguze...!



Aliishia kuniambia tu kwamba kwao ni dodoma mpwapwa, Sikujuwa kwamba Deju atakuja kugeuka nyoka mwenye sumu kali ya kuniathiri maishani mwangu..! Mwanaume huyu nimedumu nae kwa muda wa takribani miaka mitatu ikafikia kipindi namuacha na mdogo wangu wanatoka nae mimi napumzika wnaenda waendako wanakula bata mpaka basi, wakati huo mdogo wangu alikuwa akiishi gongo la mboto kwa Rafiki yangu wa kike ambye ni mwanamitindo. Kwahiyo kila wikiend alikuwa akija kunitembelea nyumbani kwangu ndipo Deju alipopatia fursa.

0 comments:

Post a Comment