+10 344 123 64 77

Sunday, September 13, 2015

BASATA YAZAUIA LUGHA CHAFU WAKATI WA KAMPENI........

Katibu Mkuu Mtendaji Baraza la Sanaa la Tanzania (BASATA), Geofrey Ngereza.
BASATA YAONYA LUGHA CHAFU, MAADILI HUSUSAN KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Katika siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la wasanii kuvunja maadili, kukaidi adhabu na kutumia lugha chafu kwa makusudi katika kazi za Sanaa hususan muziki hali ambayo imezua malalamiko, masikitiko na hofu kwa jamii ambayo ni walaji wa kazi za Sanaa.
Lugha hiyo chafu ambayo inajidhihirisha kwa matusi ya wazi, maneno ya uchochezi, kashfa, kejeli, dharau na udhalilishaji wa kada mbalimbali za kijamii wakiwemo viongozi wa kitaifa inaonesha wazi kulenga katika kuigawa jamii na kufifisha amani, upendo, uzalendo na ustaarabu tuliokuwa nao watanzania. Ieleweke kwamba kwa mujibu wa misingi ya Sanaa Duniani

0 comments:

Post a Comment