Msanii mkongwe wa filamu, Halima Yahya maarufu kama Davina, amesema katika maisha yake ya sanaa ya uigizaji hapendi scenes za mapenzi hasa hasa zile zinazomtaka aonekane akishikwa shikwa kitandani.
Muigizaji huyo ambaye ni mama wa watoto watatu, amekiambia kipindi cha Papaso cha TBC FM kuwa scenes hizo humpatia wakati mgumu wakati anapopewa ili avae uhusika.
“Scenes za mapenzi yaani ile kushikwa shikwa wakati upo kitandani sipendagi,” alisema kwa kicheko.
“Sio kwamba nachukia mapenzi ndiyo yanayoendesha dunia na movie nyingi lazima viwepo hivyo vitu. Nazungumzia yale mapenzi unacheza labda upo na boyfriend au sijui mume wako na mnatakiwa muonekane mnashikana shikana. Lakini tuna vitu mnaweza fanya halafu mtazamaji akaelewa huyu ni mtu na mke wake. Mimi kama movie yangu siwezi kutengeneza au kuonyesha watu wanalala wanashikana kwa sababu bado hatujafikia huko,” alisisitiza Davina.
Katika hatua nyingine Davina alisema anatarajia kuanzisha kipindi cha runinga kiitwacho ‘Udaku Magazetini.’
0 comments:
Post a Comment