Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live, Alikiba almesema wimbo huo hajamuimbia Jokate na wala hajawahi kumuimbia mtu yeyote, bali aliimba kwa ajili ya mashabiki wake.
” Sijamuimbia mtu yeyote kwa kweli, mi nimeimba kwa ajili ya mashabiki wangu, kwanza sijawahi kumuimbia mtu kabisa, sijawahi, so ni kwa ajili ya mashabiki wangu”,.
Lakini pia Alikiba alisema kuwa kitendo cha kuwataja wasanii wa Filamu Wema Sepetu na Lulu kwenye wimbo huo, ilikuwa ni suprise, hivyo wenyewe hawakujua kuwa wameimbwa, isipokuwa alishawahi kumdokeza Wema Sepetu ambaye ametaja kuwa ni rafiki yake mkuabwa.
“Wenyewe walikuwa hawajui kuwa nimewaimba, ila Wema nilimwambia siku moja kuwa bichwa nina suprise yako, ila Lulu sikuwahi kumwambia na hata sijui ameipokeaje, ila naamini kaipokea fresh”, alisema Alikiba.
Kitu ambacho bado kinawapa kigugumizi watu ambao walikuwa wakifuatilia kipindi hicho, pale aliposhindwa kuchagua kati ya Wema Sepetu na Jokate, na kusema anawachagua wote, na kuzidi kuweka hali ya sintofahamu kwa wawili hawa (KIba na Jokate) huenda bado wako pamoja.
0 comments:
Post a Comment