Msanii Alikiba amefunguka na kusema kwa mafanikio aliyopata toka amerudi kwenye muziki tena ndani ya muda ni mfupi ni sawa na kuchana msamba kwake maana siyo hatua za kawaida.
Alikiba alisema haya kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusisitiza kuwa yeye kusaini mkataba na kampuni ya ‘Sony Music’ jambo kubwa sana katika maisha yake ya muziki.
“Kiukweli toka nimerudi rasmi kwenye game na kutoa wimbo wa Mwana mashabiki walipokea vizuri sana Africa Mashariki, na kadili nilivyokuja kutoa wimbo mwingine wa Chekecha walizidi kuongezeka mashabiki na kujiona nina mashabiki wengi, hivyo kuja kusaini mkataba na ‘Sony Music’ ndani ya muda mfupi hivi kwangu mimi najiona ni kama nimepiga msamba maana siyo hatua za kawaida” alisema Alikiba.
Mbali na hilo Alikiba alimuombea msanii Diamond Platnum kwa watanzania ili wampigie kura kwenye tuzo anazoshiriki sasa na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo hivyo watanzania wampigie kura ili aweze kushinda.
eatv.tv
0 comments:
Post a Comment