Bado headlines za usajili zinazidi kuchukua nafasi barani Ulaya, tayari tumeshuhudia mastaa kadhaa wakivihama vilabu vyao na kujiunga na vingine, kwa upande wa Englandjina la winga wa kiwamataifa wa Algeria anayeichezea klabu ya Leicester City Riyad Mahrez limerudi tena kwenye headlines za usajili.
Ufaransa kupitia mtandao wa EuroSport wameandika stori kuwa winga huyo amesema anataka kujiunga na Arsenal ya London na sio Chelsea, kwa mujibu wa EuroSportMahrez ana lengo la kujiunga na Arsenal ila hajataka kuweka wazi.
Licha ya mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha kutangaza wiki kadhaa kuwa Mahrez ataendelea kubakia King Power, EuroSport wamezidi kuzipa uzito headlines za staa huyo kuhama King Power na kujiunga na Arsenal.
0 comments:
Post a Comment