MWANADADA anayefanya poa kwenye game la muziki Bongo, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefungukia maana halisi ya tatuu zake mpya alizojichora baada ya kufuta zile za awali ikiwemo ile ya X- wake, Nuh Mziwanda.
Shilole aliiambia safu hii kuwa, mbali na zile zinazosomeka kama jina lake la Shishi, zile za Kichina ni alama za kimuziki ambazo zinaonesha jinsi anavyoipenda kazi yake.
“Tatuu zangu zimechorwa kwa lugha ya Kichina na Kiingereza, hii ya bega la kulia ni jina langu la Shishi Baby na hizi nyingine za Kichina ni ala za muziki kuonesha hisia zangu za dhati juu ya muziki na nimefuta zile za zamani zote,” alisema Shilole.
0 comments:
Post a Comment