NI Kama wewe ni moja ya watu wanaomfuatilia kwenye mtandao picha wa Instagram, utakuwa umejionea ni kwa kiasi gani staa mrembo wa Bongo Movies, Jacqueline Wolper anapenda MITIND0.
Akizungumza na mtandao wa bongo 5, ambao ulitaka kujua mapenzi yake kwenye fashion na kama anapata changamoto kuhakikisha anapendeza muda wote.
>>>Ni hobby sana sana, hakuna challenge kwasababu kila mtu anapenda kitu chake<<<,” amesema Wolper.<<< Mimi napenda kuvaa.”
Katika hatua nyingine Wolper amesema ameshafikiria kuja na kipindi cha TV cha masuala ya fashion lakini anahitaji kujifunza zaidi.
“Movie ni kazi yangu ambacho ni kipaji changu lakini hivyo vingine nina idea navyo kidogo tu na kuna watu ambao tayari wameshaingia kwahiyo vitu vingine mpaka nijifunze labda ndio niingie.”
Wolper pia alisema bado amesimama kufanya filamu kutokana na sababu mbalimbali za kwenye tasnia hiyo japokuwa amekili kuwa kuwakosesha vitu mashabiki wake kwa kipingi hiki ila watajua ila watakuja kujua tu sababu ya yeye kusimama.
0 comments:
Post a Comment