BAADA ya mashabiki wake kumtaka aongeze mtoto wa tatu, msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni muigizaji, Khadija Shaban (Keisha), ameibuka na kuweka wazi kwamba hana mpango wa kuzaa tena kwa sasa.
Keisha aliliambia gazeti la Mtanzania kuwa, sababu kubwa inayomfanya asitamani kuongeza mtoto kwa sasa ni kutokana na kuwa na watoto wawili wa kiume wenye umri mdogo.
“Kama nitabeba ujauzito mwingine kwa sasa mimi na baba yao tutakuwa hatuwatendei haki hawa watoto wetu, wanahitaji muda wa kukua zaidi ndipo tufikirie kuongeza wenzao wengine,” alisema msanii keisha
0 comments:
Post a Comment