Kutoka Mtandaoni: Kupitia ukurasa wake mtandaoni, staa wa Bongo movies, Aunty Ezekiel aliweka picha hiyo hapo mtandaoni akiwa na staa mwenzake, Monalisa nakuwauliza mashabiki kama wawili hao wanafanana huku akikumbushia msala mabao aliufanya yeye na kukamatwa Monalisa.
“Eti tumefanana???Nishawahi kukosa mm akakamatwa yy jaman!!! Mi sijui ww je?Mtag kama unajuana nae bac....!!!”- Aunty aliandika.
Monalisa Ajibu
Monalisa naye kamjibu Aunty kwa kuweka picha hiyo kwenye ukurasa wake na kusema anaukumbuka ule msala, na kukataa kiutani kuwa hawafanani.
“Yaani siwezi sahau nilivyosingiziwa ule msala wako wakaning'ang'ania mimi jamani duh!sielewi wanatufananishaga vipi?maana mi mrefu we mfupi,mi mweusi sana we mwenzangu mng'avu,kabila tu ndo tunafanana Aunty Ezekiel haya na kilichofanya leo unikumbuke asubuhi asubuhi nini?? Huyo cookie atafanana na mimi nakuambia”, Monalisa aliandika.
0 comments:
Post a Comment