NI Muigizaji mkongwe wa Mzee Majuto amejidhatiti zaidi kwa kufungua kampuni yake mwenyewe ya filamu.
Mzee Majuto ameiambia Bongo5 kuwa huo ni mwanzo wa mipango yake mikubwa.
“Sasa hivi na mimi nina camera zangu, nina watu wangu karibu 75 nimewafundisha vijana ili kuwapa ajira na kweli wamejiajiri, tunatengeneza mikanda, tunauza wenyewe, tunakaa mezani tunagawana. Kwahiyo tuna nguvu,” amesema Majuto.
“Halafu mimi mwenye pia nimejiweka vizuri, nimenunua shamba, nikalitengeneza vizuri, nikaweza mabanda ya kuku (Tanga) na nataka nianze na kuku ELFU SABA na mbuzi. Watoto pia wanasoma shule nzuri, namshukuru Mungu kusema ukweli.”
0 comments:
Post a Comment