+10 344 123 64 77

Tuesday, May 26, 2015

USWAZI NI KWETU!!!! RIYAMA AJIVUNIA MANENO YA KIUSWAZINI>>> HEBU YAANGALIE MANENO HAYA

Riyama Ajivunia Maneno ya Kiswazi

     


    NI Staa wa Bongo Movies, Riyama Ally, ameibuka  na kusema anajivunia  kuwa na manenona misemo ya kiswazi  ambayo huzungumzwa na wanawake wanaishi sehemu  za uswahilini ndiyo maana amekuwa akishirikishwa kwenye Filamu nyingi.
    Akizungumza  na  Tanuru la Filamu jana, Rayama  alisema  kuwa filamu mpya iitwayo WOGA  ambayo ipo madukani sasa imesababisha watu wengi wahisi kama ndivyo alivyo hata akiwa nyumbani kwake kwa sababu uhusika alioubeba  huku unaonekana ndivyo tabia yake.
    >>>>>>>>NinA  kila sababu ya kujivunia maneno  machafu  ya uswahilini kwani hayo ndivyo  yananifanya nipate mialiko  mingi ya kuigiza  kama  nilivyoshirikishwa  kwenye filamu  hii ya WOGA ambayo ni mejitahidi  kuuvaa uhusika  na kitendo hiki ndicho kinanipa heshima badala ya kuwa na skendo kama wafanyavyo wasanii wengine" alisema Riyama.
    Mbali na Riyama wasanii wengine waliocheza kwenye filamu hiyo inayosambazwa na Freshas Campany Ltd ni David Justine, Hashim Kambi, Abdalla Hamis na Mohamed Fungafunga. na hizo ndo swaga za kiuswazi mazeeeeeee

    0 comments:

    Post a Comment