NI Jina la kocha wa zamani wa Liverpool Rafa Benitez limetajwa kuongoza orodha ya makocha wanaotarajiwa kuwania nafasi ya kumrithi kocha wa sasa Carlo Ancelotti baada ya Mtaliano huyo kuwa hatarini kufukuzwa kazi kwa mujibu wa ripoti kadhaa zilizoonekana kwenye vyombo vya habari .
Benitez ambaye kwa sasa anafundisha klabu ya Napoli ya nchini Italia amepewa kipaumbele kama chaguo la kwanza la kurithi nafasi ya Ancelotti na rais wa Real Madrid Florentino Perez ambaye tayari inasemekana kuwa amefikia uamuzi wa kumfukuza kazi Ancelotti .
Benitez hayuko peke yake kwenye orodha hiyo ambayo pia inamjumuisha kocha wa zamani wa Borrusia Dortmund Jurgen Klopp ambaye atakuwa huru baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi ya Ujerumani akiwa tayari ametangaza kuachana na klabu yake .
Rafa Benitez anaonekana pia kuwa chaguo la mashabiki wa Real Madrid ambao wengi wanamtambua kama mwenzao kutokana na mizizi aliyo naye ndani ya klabu hiyo .
0 comments:
Post a Comment