+10 344 123 64 77

Thursday, June 18, 2015

DAH!!! AIBU SANA MAMA...BABA...NA WATOTO KULALA KATIKA CHUMBA KIMOJA KWA SABABU YA KUOFIA UCHAWI.....SOMA ZAIDI HAPA

Familia ya Zidadu Kasimu [34] inayoishi Mlandizi, Pwani inakumbwa na mauzauza nyakati za usiku kwenye nyumba yao baada ya wageni wanaofika na kulala vyumbani kusimulia visa vya kutisha vinavyohusisha ushirikina.
Akizungumza  mwishoni mwa wiki iliyopita, Zidadu alisema vitimbwi hivyo vilianza mwaka 2004 baada ya wageni wake kusimulia ndoto za ajabu, majinamizi, kuguswa na mtu asiyeonekana na kusikia sauti za watu wakitwanga mpunga.
>>>Yaani kaka ilifikia hatua wageni wakija wanakimbia usiku, wengine wakiamka wanaondoka bila kuaga na hawarudi tena, sasa tumefunga vyumba hivyo tunalala wote chumba kimoja ambacho hakina mauzauza<<< alisema Zidadu.

Mke wa Zidadu, mama Mau alisema licha ya mauzauza, pia kuna wakati fedha zao hupotea kiajabu na kuna siku walishangaa kuona mfupa ukitoka chooni na kuingia uvunguni mwa kitanda jambo lililowashtua sana 

0 comments:

Post a Comment