+10 344 123 64 77

Monday, June 8, 2015

DINNAH & ZAMARADI MTETEMA!!! HATUNA UGOMVI SISI.......... BOFYA HAPA KWA HABARI ZAIDI

Dinah Marious: Sina Ugomvi na Zamaradi Mtetema

 NI Aliekuwa mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na redio Clouds FM, Dinah Marious mbali na kuelezea kile kinachoendelea kati yake na  uongozi wa redio hiyo, Dinah ameweka wazi kuwa hana ugomvi wowote na mtangazaji mwenzie, Zamaradi Mtetema.
Dinah kupitia ukurasa wake mtandaoni alianza kwa kuelezea hali halisi kati yake na mwajiri wake.
>>Katika haya maisha hamna kitu kibaya kama kumuonea na kumnyanyasa mtu ambaye hana hatia.Kwa kutumia cheo,madaraka,nguvu na nafasi uliyonayo ukiamini huyo mtu hana uwezo wa kukufanya lolote
Tunaishi katika dunia ambayo binadamu wamekosa utu na imani.Binadamu wamekuwa wanyama na makatili kuliko wanyama wenyewe.Unaweza ukakutana na simba na chui porini mkakaa mkatia story lakini sio binadamu.
Unafanyiwa unyama eti kisa wanataka revenge kwa mtu wako wa karibu.Ambae revenge hiyo wala haimuathiri lolote zaidi ni kukutesa wewe kisaikolojia siku hadi siku.
Mbaya zaidi sikustahili miaka yote nimejituma,nimejitoa,sijawahi kumvunjia heshima alokuwa juu yangu kwa ngazi zoote.

Ndugu zangu nimeishi kwa muda mrefu katika huzuni,msongo wa mawazo.Na hapa niliponimedevelop na vidonda vya tumbo.Nimekuwa na kitu kifuani kimenikaaa kila siku nahisi nisiposema nitakufa.Ningekuwa nimetendewa haki isingeniuma wala kunisumbua ni kwa sababu nimeonewa sanaa tena katika kipindi kibaya sana.
All this time nimekuwa mnyenyekevu na najichekesha nakujitabasamisha machoni pa watesi wangu.Na wao wakiendelea kunikanyagia chini bila huruma huku wakinichekea.

Leo nimeamka nina huzuni sana sana na ninahuzunika hasa ninapokutana na msg za kuniuliza niko wapi?mbona sisikiki??
Mimi bado ni muajiriwa na jinalipwa mshahara ila nimewekwa benchi tu," Dinah alieleza.

 
Kisha akaweka wazi kuwa hana ugomvi na Zamaradi
>>>Kuna kitu naomba nikiweke clear kumekuwa na maneno mengiiiiii yanazunguka kuwa nina ugomvi na Zamaradi.Mimi sina ugomvi na Zamaradi sijui ndio amechangia mimi kutolewa kwenye leo tena.Thats not true wala nguvu hiyo hana.Sijajua why watu husema hivyo ila sina ugomvi nae.Hata yeye anajua hatuna ugomvi wowote.Nilipotoka pale niliamua kubadili mfumo wangu wa maisha hivyo hatuna ukaribu kama zamani.Ila haimaainishi tuna ugomvi<<<.
                                                                  

0 comments:

Post a Comment