NI Ishu ya mastaa wa Marekani kufanya vurugu wanapokuwa kwenye shoo si jambo geni mbele ya mashabiki wao na ukimzungumzia staa kama Chris Brown amekua akikumbwa na matukio hayo mara kwa mara.
Leo kwenye headlines member wa kundi la G- Unit, ZE Game amesikika kwenye mkasa uliomkumba yeye na polisi huko Los Angeles, Marekani mapema mwezi March mwaka huu.
Rapper huyo alifunguliwa mashtaka baada ya kuingia kwenye mgogoro na polisi aliyekua nje ya kazi wakati wakicheza mpira wa kikapu wakiwa kwenye uwanja wa basketball kisha kumpiga ngumi tukio lililonaswa na baadaye kurushwa kwenye mtandao wa Youtube.
Japo tukio hili lilitokea tangu mwezi March, lakini polisi wamesema kwamba wameamua kufungua mashtaka baada ya video hiyo kusambaa sana kwenye mitandao na kuwadhalilisha.
0 comments:
Post a Comment