+10 344 123 64 77

Friday, June 5, 2015

IN SPORT.....IRINA SHAYK!!!!.... HUENDA NI CHANZO CHA BLATTER KUMPOTEZA RONALDO....... FUATILIA HAPA

  

    NI  Mambo yanazidi kumuendea vibaya Raisi wa FIFA, Sepp Blatter. Ikiwa imepita siku kadhaa tu tangu atangaze kwamba ataachia ngazi kwenye uongozi wa taasisi hiyo ya masuala ya soka kutokana tuhuma za rushwa kuzidi kuiandama taasisi hiyo.
Leo hii zimetoka taarifa nyingine ambazo zimeibua tetesi za siku nyingi kwamba Raisi huyo wa FIFA alikuwa hana uhusiano mzuri na mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo.
Gazeti lenye heshima kubwa nchini Spain – El Mundo limeripoti kwamba aliyekuwa mchumba wa Ronaldo, Irina Shayk alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Sepp Blatter katika vipindi viwili tofauti.
El Mundo linaripoti kwamba Blatter alikuwa na mahusiano ya muda mrefu na Mrembo huyo wa kirusi, baada ya kuachana na mcheza tenis Ilona Boguska lakini kabla ya kukutana na mwanamama  Linda Barras, 50. 
Habari hiyo ya Irina na Blatter imeandikwa kwenye na mwandishi wa gazeti la El Mundo Rosalia Sanchez.
Anaelezea kwamba taarifa hiyo ya siri ya mahusiano ya Irina na Mzee Blatter ilipata kutoka kwa chanzo chake cha kuaminika wakati anafanya uchunguzi wa taarifa za rushwa na mahusiano zinamhusu boss huyo wa FIFA.
Uhusiano wao inasemekana ulianza mwaka 2002, wakatengana na kuja kuendelea tena mwaka 2014, wakati Irina akiwa bado na mahusiano na Cristiano Ronaldo ambaye walianza mwaka 2010 mpaka mwanzoni mwa mwaka huu walipotangaza kuachana.
Msemaji wa Irina Shayk alipoulizwa juu ya tuhuma hizi, hakujibu lolote. Hii ni kwa mujibu wa Dailymail ya Uingereza.

0 comments:

Post a Comment