NI STAA wa filamu za Bongo, Adam Haji ‘Baba Haji’ leo anatarajia kufunga ndoa kwenye Msikiti wa Bungoni jijini Dar na mchumba ‘ake wa siku nyingi, Latifa Sharji.
Baba Haji alisema anamshukuru Mungu kufikia hatua hiyo kubwa katika maisha yake kwani ni jambo alilokuwa akilisubiri kwa miaka kadhaa.
>>Yaani namshukuru Mungu, nampenda mpenzi wangu Latifa na namshukuru kwa kunikubalia kufunga ndoa kwani wengine huishia njiani katika safari yao ya mapenzi<< alisema Baba Haji.
0 comments:
Post a Comment