NI YULE Staa wa Bongo Movies, Riyama Ally amesaini mkataba mnono wa kucheza filamu na kampuni maarufu ya kusambaza filamu nchini Kenya.
Riyama alisema kuwa amefanya mazungumzo na kampuni hiyo mjini Mombasa na tayari wameshaanza kufanya kazi na kumlipa kitita kinono cha fedha ambacho hakukitaja.
Aidha amesema kuwa wadau wengine wa filamu nchini Kenya wametangaza dau kubwa zaidi ili msanii huyo aweze kucheza tamthilia zinazorushwa kwenye TV mbali mbali nchini humo.
0 comments:
Post a Comment