Christy Sims ni mwanadada ambaye maisha yake yalibadilika ghafla baada ya aliekuwa mpenzi wake wa muda mrefu kumuachia majeraha ambayo hatokuja kuyasahau maishani.
Akiwa na miaka 40 Christy amelazimika kuishi na makovu baada ya kumwagiwa tindikali na ex-boyfriend wake kwa sababu tu ya wivu wa mapenzi, kumhisi kuwa anatembea na mtu mwengine.
Haya yote yalitokea weekend moja ya mwaka 2013 nyumbani kwa mpenzi wake ambaye aliamua kumwagia dada huyu tindikali usoni, kifuani na mikononi kitendo kilichosukumwa na hasira kali za wivu.
Christy alipiga kelele nyingi na kuomba msaada lakini boyfriend wake aliamua kumuacha aungue mpaka watu wa huduma ya kwanza walipofika na kushangazwa kwa nini boyfriend huyo hakuchukua hatua za kumpatia girllfriend wake huduma ya kwanza.
0 comments:
Post a Comment