+10 344 123 64 77

Monday, August 10, 2015

MAJANGA TENA HAYA!!!!! YOTE HAYA NI KWA AJILI YA VIKOBA.......SOMA ZAIDI HAPA



MAJANGA! Mwanamke mmoja, Catherine Melzedeki mkazi wa Mzinga, Kitunda jijini Dar ambaye ni Mweka Hazina wa kikundi cha Vikoba amezua balaa baada ya kukombwa samani za ndani kufuatia kushindwa kulipa hela ya upatu inayofikia shilingi milioni 1.2.
Tukio hilo lilitokea Agosti 7, mwaka huu nyumbani kwa Catherine baada ya wanachama wa kikundi hicho cha Yosefu Microfinance kugundua kuwa mwenzao huyo amechikichia kiasi cha shilingi milioni mbili baada ya kuwazungusha katika kulipa michango ya kila mwezi na kusababisha deni kuwa kubwa.
Katibu wa kikundi hicho, Grace Samweli alisema waligundua wizi huo baada ya kumfuatilia Catherine kwa miezi mitatu bila kutoa mchango wake kwa kikundi kitu kilicholazimu uongozi kumpa barua kwa vipindi vitatu tofauti akitakiwa kutoa maelezo bila mafanikio.
“Tulipokuwa tukija nyumbani kwake mumewe na watoto walituambia anaumwa kaenda hospitali, kila siku stori ni hiyohiyo. Hasira zilizidi baada ya afisa wa kikundi chetu kutoka makao makuu kutukata shilingi elfu 90 kila mmoja ili kufidia deni la huyu mama, tukaamua tuchukue vitu vyake ili tufidie,” alisema katibu huyo na kudai kuwa pamoja na kuchukua vitu hivyo bado deni halijaisha.
Kana kwamba haitoshi, akina mama wa kikundi kingine kiitwacho Mubatiki nao walijitokeza na kudai Catherine alikuwa ni mwenyekiti wa kikundi chao na amewadhulumu shilingi milioni 8.
“Leo ndiyo tumegundua kumbe mwenyekiti wetu alikuwa kwenye kikundi kingine na anadaiwa kama sisi tunavyomdai. Wenzetu wanachukua vitu vyake, sasa kwetu sijui tutachukua nyumba kabisa, maana tunamdai shilingi milioni 8 ambazo hadi leo hajatulipa na amekuwa akitukimbia,” alisema katibu Christina Paschal na kuongeza kuwa, hata hivyo sakata lao wamelipeleka mahakamani.
Waandishi wetu wakiwa eneo la tukio walishuhudia samani za ndani na vifaa vya umeme vikichukuliwa na kuachiwa kitanda alichokuwa amekilalia kwa kujifunika na neti.
Aidha, mjumbe wa mtaa huo, Asha Matimbwa alisema alipata malalamiko ya kikundi hicho mapema na alishamtaarifu mhusika kuhusu suala hilo

0 comments:

Post a Comment