Naweza kusema pia penzi ni kama siti ya daladala, ukishuka wewe mwingine anakaa. Wakati mwingine kuna kuwahiana au kupokonywa. Hapa namaanisha kwamba katika mapenzi kama utakuwa na moyo mdogo wa kutikiswa na vishawishi na wewe unafungasha virago vyako kurudi kwenu, unakuwa unafanya makosa.
Usikubali kuachia ngazi mapema, ng’ang’ania na pigania penzi lako kwa nguvu, usiruhusu kupokonywa kizembe.Kama utaruhusu kutikiswa na ukatikisika unakuwa unakosea sana, utapokonywa wangapi? Haiwezekani mtu aje akutoe kirahisi kwenye penzi uliloanza nalo likiwa changa na leo umelikomaza ili ule matunda mjinga f’lani anaingia kati na kujitamba kwamba yeye ndiye anapendwa kuliko wewe.
Kama alikuwa anapendwa kwa nini hakuwekwa ndani? Hilo ni moja ya swali la kujiuliza, wewe ulipendwa na kuchaguliwa ndiyo maana ukawekwa ndani, haijalishi umefunga ndoa ya kimilia, serikalini, kanisani, msikitini au hujafunga ndoa ilimradi umewekwa ndani.
Muombe Mungu lakini pia kuwa mvumilivu na mshauri mwenzi wako haijalishi ni mbishi kiasi gani, kama utazungumza ukweli kwake utaona taswira yenye kukuashiria kuwa ulilomwambia kalielewa.
Yawezekana ulisafiri mwezi mmoja au zaidi ukasikia au ukagundua mwenza wako alikusaliti, umia, kubali kupepesuka ila usianguke.Ni kweli usaliti unauma sana na kama watu watajua udhaifu wako watakuingilia na utashangaa unajiweka kando kwa mtu ambaye huenda Mungu alikuwa kapanga muwe pamoja milele.
Ndiyo maana leo nikaona nikutie moyo kwa kukuambia kuwa, kwa mtu uliyetokea kumpenda usikubali mtengane kirahisi. Pigana mpaka pale ambapo utaona kabisa kwamba hakuna jinsi ndiyo unaweza kufanya maamuzi magumu.
Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.
Ni hayo tu kwa leo, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine.
0 comments:
Post a Comment