Pambano la Floyd Mayweather na Manny Pacquiao May 02 2015 lilivunja rekodi nyingi ikiwemo ya mauzo ya Ticket, ticket ziliuzwa kati ya Dola 1,500 na Dola 10,000 lakini ndani ya saa mbili tu ziliuzika zote !!
Tunahesabu saa chache zilizobakia kuanzia sasahivi kabla ya kushuhudia pambano jingine la Mayweather na Andre Berto… mauzo ya ticket unajua yakoje?
Wanahabari wamekatisha mtaani na hawajakosa cha kuripoti, pambano la kesho September 12 2015 ticket zinauzwa kati wa Dola 150 na Dola 1,500 lakini mpaka sasa hivi ticket za Dola 150 pekeyake ndio zinaelekea kuisha, nyingine zote mambo bado hayasomeki !!
Pambano halina mvuto? Wachambuzi wa mambo wanasema Rekodi ya Andre Berto inaonesha amecheza mapambano 33, kashinda mapambano 30 na kushindwa matatu.. hiyo sio Rekodi kubwa sana ya kumpambanisha na Mayweather ambae hajawahi kushindwa hata pambano moja kati ya 48 aliyowahi kucheza tangu amekuwa Bondia professional.
Ripoti ya Jumanne September 08 2015 ilionesha kulikuwa na siti 2,100 ambazo zilikuwa bado wazi katika Ukumbi wa MGM Garden Arena, Las Vegas Marekani.. hiyo inamaanisha Ticket hizo bado hazijauzwa kabisa !!
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa
0 comments:
Post a Comment