+10 344 123 64 77

Saturday, September 5, 2015

HAYA NDIO MANENO YA Kylie Jenner KUHUSU WATAFUTA UMAARUFU INSTAGRAM..BOFYA KUJUA ZAIDI HAPA

Tunapowaona mastaa kwenye mitandao na social networks huwa tunaona na kuhisi kuwa kila kitu kuhusu maisha yao kimekamilika na wakati mwengine huwa tunahisi kuwa mastaa wengi hutumia nafasi walionayo kufanya chochote kile wajisikiacho kufanya kiwe kizuri au kibaya.
Je hii ni kweli kwa kila mtu? model na social media personality Kylie Jenner haamini kuwa kila mtu aliyemaarufu anatumia nafasi yake vibaya… siku chache zilizopita Kylie Jennermwenye followers  million 34 Instagram aliandika…
kyliejenner2
====>>> “Kwa siku sita zijazo, nitakuwa nashare na nyinyi stori za msahujaa 6 ambao kupitia wao nimejifunza vitu vingi kuhusu #kusemwa vibaya na kutumia nafasi walizo nazo kubadilisha mitazamo ya maisha”.<<< @kyliejenner.
Siku iliyofuata Kylie Jenner alishare picha nyingine na kusema; >>>“dada huyu alianza kusemwa vibaya alivyojiunga na chuo, lakini leo namuita shujaa kwa sababu aliweza kumudu kuishi na kusonga mbele… wakati mwengine inaniwia vigumu kupotezea zile comments zote mbaya zinazoandikwa na watu kwenye page yangu…#I love u Renee #MimiNiZaidi ya comments mbaya zinazoandikwa”<<< @kyliejenner.
Kylie Jenner akamua kufunguka kuhusu matatizo anayoyapata kila siku kutoka kwa washambuliaji wake kwenye mitandao ya kijamii, alisema anaumia na wakati mwengine huwa anashindwa kuvumilia na anajikuta analia…
“Watu ni wepesi sana kuona na kuhukumu vitu kwa juu juu tu, na watu ni wepesi sana kunisema vibaya kila siku na mara nyingine nashindwa kuvumilia, navunjika moyo, naumia, nalia” <<< @kyliejenner.

0 comments:

Post a Comment