Ikiwa ni siku chache zimepita toka staa wa klabu ya Real Madrid ya Hispania na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo kutangaza majina matano ya wachezaji wanaochipukia ambao yeye anaamini watafanya vizuri, November 12 beki wa klabu ya FC Barcelona yaHispania na timu ya taifa ya Hispania Gerrard Pique ametangaza first eleven ya wachezaji 11 bora.
Beki huyo wa FC Barcelona alitaja first eleven yake yaani wachezaji 11 ambao anaamini wanapaswa kuingia katika kikosi cha kwanza cha wachezaji wa Dunia ila kitu kilichowashangaza wengi katika list hiyo ni kukosekana kwa jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo.
Pique alitaja majina ya David de Gea wa Man United, Sergio Ramos wa Real Madrid,John Stones wa Everton ya Uingereza, Paul Pogba wa Juventus, Cesc Fabregas waChelsea lakini alijumuisha majina sita ya wachezaji wenzake wa FC Barcelona na likiwemo jina lake Luis Suarez, Neymar, Lionel Messi, Andre Iniesta na Busquets.
Hii first eleven ya Gerrard Pique imewashangaza wengi baada ya Uingereza kuchukua jina la mchezaji mmoja pekee la John Stones kutoka Everton huku wengine wakiuliza mshambuliaji kama Wayne Rooney ni kweli hawezi kustahili kuwa katika list hiyo.
0 comments:
Post a Comment