Wakati mwingine katika maisha unaweza pata matatizo ya kiafya na baadhi ya wataalam wanaweza kusema kuwa unaumwa hiki lakini ukawa ni uchunguzi batili. November 12 beki wa kimataifa wa Ufaransa aliyewahi kuichezea Man United ya Uingereza kwa miaka 7Patrice Evra amegundua chakula kilichokuwa kina mdhuru wakati yupo Man United.
Evra alikuwa akila mayai kila siku licha ya kuwa alikuwa hajui kama anaaleji nayo kitu ambacho kilimpelekea kila siku kutapika mazoezini wakati yupo Man United, aliwahi kwenda hospitali wakati yupo Uingereza lakini aliambiwa kuwa ana tatizo la vidonda vya tumbo kitu ambacho sio kweli na tatizo lake limepatiwa majibu akiwa Juventus ya Italia.
“Nilipo jiunga na Juventus ndio waliniambia kuwa nina allergic na mayai ila nilikuwa nakula kila siku wakati nikiwa Man United nilikuwa nikitapika mazoezini lakini nilipoenda hospitali wakaniambia ninacheza soka huku nikiwa na vidonda vya tumbo sema nilikuwa na bahati kwa sababu vilikuwa havipo katika hali mbaya” =====>>> Evra
Patrice Evra ambaye ana umri wa miaka 34 alijiunga na Juventus ya Italia mwaka 2014 katika dirisha la usajili la majira ya joto na amecheza jumla ya mechi 47 toka ajiunge na Mabingwa hao wa Italia.
0 comments:
Post a Comment