Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya HispaniaCristiano Ronaldo anaripotiwa kutumia mkwanja mrefu kununua ndege binafsi, Staa huyo anayeongoza katika list ya rekodi ya watu maarufu wanaongoza kupata likes nyingi katika mtandao wa facebook amenunua ndege binafsi aina ya Gulfstream G200 Business Jet.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 anatajwa kununua ndege hiyo kwa thamani ya pound milioni 13.5 ambazo ni zaidi ya bilioni 44 za kibongo kwa ajili ya kuzunguuka sehemu mbalimbali duniani kuhusiana na mipango yake ya kujitanua kibiashara, ndege ya staa huyo inatajwa kuwa na uwezo wa kubeba watu 8 hadi 10, jiko la umeme, bafu, friji, makabati, simu na internet.
Staa huyo ambaye anaonekana kujiimarisha zaidi kibiashara tayari amezindua movie ya maisha yake halisi aliyoizindua hivi karibuni Uingereza ila mwaka 2015 alitajwa kuzindua perfume, brand ya viatu vyake.
0 comments:
Post a Comment