Kama ambavyo dirisha la dogo la usajili la Ligi Kuu soka Tanzania bara linafungwa December 15, yaani siku moja imesalia kabla ya dirisha kufungwa, barani Ulaya bado homa ya usajili wa dirisha dogo la mwezi January inazidi kushika kasi, mengi yanaandikwa na mengi tunasikia. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee stori 5 zilizoingia katika headlines ya usajili December 13.
5- Mke wa Pep Guardiola ameizungumzia Man United
Klabu ya Manchester United inahusishwa kwa karibu na mpango wa kutaka kumchukua kocha wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani Pep Guardiola kuja kuifundisha timu yao, stori ni kuwa mke wa kocha huyo amezungumza kwa mara ya kwanza kuwa anapenda kuishi jiji la Munich na sio Manchester.
Kwa taarifa zisizo thibitika ni kuwa uongozi wa Man City ambao pia unamtaka Pep Guardiola, unatajwa kupewa masharti na kocha huyo kumsajili staa wa Alex Sanchez kabla ya yeye hajasaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo, kwani Sanchez yupo katika mipango yake.
0 comments:
Post a Comment