Wiz Khalifa akiwa katika pozi.
SIKU zote mashabiki huwa kichocheo cha bifu nyingi zinazozuka miongoni mwa wasanii.
Bongo suala hili limekuwa kitu cha kawaida sana kwani kupitia mitandao, yapo makundi ya mashabiki ambayo kazi yao kubwa ni kushambulia upande wa pili wa msanii ambaye wanaona ni mpinzani wao.
Kanye West akiwa katika pozi.
Sikia hii:
Wakati mashabiki wa Kibongo wakichukulia fasheni kwa mastaa wao kuwekeana bifu za wazi wazi ikiwa ni pamoja na kutukanana nchini Marekani hali ni tofauti.
Kutokana na bifu kubwa lililonoga wiki hii kati ya mastaa wa Hip Hop, Wiz Khalifa na Kanye West kupitia kurasa zao za Twitter, mashabiki wao zaidi ya watano wameamua kuligeuza bifu hilo kama sehemu ya kujiingizia kipato ambapo wamezichukua Tweets zote za bifu walizokuwa wakirushiana Kanye na Wiz kisha wakazihamishia kwenye t-shirt na kuzipiga bei.
Kati ya T-Shirt wanazoziuza jamaa hao kwa dola 25.
Jamaa hao kwa sasa wanazidi kutengeneza mkwanja mnene ambapo kwa t-shirt moja wanaiuza kwa dola 25 za Kimarekani (Zaidi ya Sh. Elfu 54 za Kitanzania).
Ugomvi wa Kanye na Wiz ulianza baada ya Wiz kuponda jina la Wave alilotumia Kanye kwenye albamu yake itakayotoka mwezi ujao aliyoiita Swish hapo awali.
0 comments:
Post a Comment