Vikao vya Bunge vimeanza Dodoma, na kila updates zinapotokea nakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba hakikupiti kitu, kuna maswali matatu alifikishiwa mezani Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano Tanzania, Kassim Majaliwa…
Kuna ahadi ya elimu bure, chakula cha wanafunzi je? Kuna ripoti ilitoka Magazetini kwamba amepiga marufuku mikutano ya kisiasa, amejibu nini? na ishu ya ‘LIVE’ kutoka Bungeni yaTBC je? Majibu niliyoyapata haya hapa.
1: >> Suala la kuzuia mikutano ya vyama vya Siasa >> ‘Nilipita Jimboni kwangu nikafanya mikutano na kwa pamoja tukishirikiana na Madiwani wa vyama vya Upinzani, tulikubaliana kwamba ni lazima tufanye kazi, nilichotamka ilikuwa ni kauli za pamoja kwa Madiwani wote kwamba siasa zikae pembeni tufanye kazi… tuliamua kufanya kazi bila kuzingatia itikadi zetu, najua utawala wa Sheria na vyama vya Siasa vina haki… niliongea kama Mbunge wa Jimbo na sio kwa cheo cha Waziri Mkuu‘- Waziri Mkuu Majaliwa Kassim.
2: >> Kuhusu TBC kufunga matangazo ya Live kutoka Bungeni >> ‘TBC haijaacha kutangaza matangazo walichofanya ni kubadili ratiba, matangazo yanarekodiwa na baadae yanarushwa… ni mpango wa Taasisi yenyewe, walipoishauri Wizara tukaona litolewe maelezo Bungeni na huo ndio msimamo wa Serikali.’- Waziri Mkuu Majaliwa.
3: >> Kuhusu chakula cha wanafunzi kwenye mpango wa ‘elimu bure’ >> ‘Iko mikanganyiko imejitokeza kwenye huu mfumo, Serikali imetangaza hakutokuwa na ada ya 20,000 kwa mwaka shule za kutwa na 70,000 shule za bweni.. shule za msingi na sekondari mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili kote ni bure… shule za Sekondari za bweni Serikali inagharamia chakula, mkanganyiko uko kwenye shule za kutwa, Wizara inaandaa utaratibu mzuri na utatoka waraka utakaoweka wazi kila kitu‘- Waziri Mkuu Majaliwa.
Hii hapa sauti ya majibu ya Waziri Mkuu Majaliwa kwenye kikao cha Bunge Dodoma
0 comments:
Post a Comment