Baada ya headlines nyingi kuandika kuhusu kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgijianayeichezea klabu ya Chelsea ya Uingereza Eden Hazard kuwa vilabu vya Real Madridya Hispania na klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa vinawania saini yake kwa karibu, klabu yake ya Chelsea imebainika kuandaa mbadala wake.
Chelsea wanatajwa kuandaa dau la pound milioni 60 kwa ajili ya kumnasa Antoine Griezmann kutoka klabu ya Atletico Madrid katika majira ya usajili ya dirisha kubwa, kamaHazard ataamua kujiunga na vilabu vya PSG au Real Madrid, Chelsea wanatajwa kuwa na maamuzi ya kumsajili Antoine Griezmann mwenye wa miaka 24 ili arithi nafasi ya Hazard.
Dau la pound milioni 60 linatajwa kuwa rahisisha Atletico Madrid kumruhusu Antoine Griezmann kujiunga na Chelsea, kwani hilo litakuwa dau la kihistoria kwa klabu hiyo, kama watafanikiwa kumuuza mfaransa huyo kwenda Chelsea ya Uingereza.
0 comments:
Post a Comment