+10 344 123 64 77

Sunday, January 31, 2016

Chopa la Doria Wanyamapori Latunguliwa, Rubani Auawa..soma zaidi hapa

a0e63c93fb79e7868c98e7e85e7e389dWaziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe akitembelea eneo la tukio.4762c1c103b4b15f688a046e2161c2ebHali ilivyokuwa eneo la tukio.010ef29dde2baf9bd5b0c6b742ad515cec3db81496098e8f4ea565c736141c62
Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu wameitungua kwa risasi helkopta ya doria ya wanyamapori katika pori la akiba la Maswa lililoko Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Kusini mwa hifadhi ya taifa ya Serengeti na kumuua rubani wa helkopita na kumjeruhi askari mmoja wa wanyamapori.
Kufuatia tukio hilo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amefika katika eneo la tukio na kusisitiza kwamba serikali kwa kushirikiana na vyombo vyote vya dola na vyombo vya ulinzi na usalama inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na uwindaji haramu wa maliasili ikiwemo Tembo ambao ni rasilimali muhimu kwa taifa na kwa uhifadhi wa taifa la Tanzania.
Waziri Maghembe ambae amefika kwenye eneo hilo ilipotunguliwa na kuikuta helkopita hiyo iliyokuwa inarushwa na kapteni Roger Gower raia wa Uingereza ambae alifariki baada ya kujeruhiwa kwa risasi amesema tukio hilo limewakera wadau wote wa uhifadhi na serikali kwa ujumla na kamwe haliwezi kuachwa lipite bila hatua madhubuti kuchukuliwa huku akiwaonya baadhi ya watumishi wa serikali na askari wa wanyamapori wanaoshirikiana na wahalifu kuwa sasa kiama chao kimefika.
Nae kamanda wa upelelezi wa Mkoa wa Simiyu, Jonathan Shana amesema tukio hilo lilitokea jana jioni wakati helkopita hiyo ikiwa katika doria baada ya kusikika milio ya risasi ya majangili katika pori hilo ambapo Tembo watatu waliuwawa na kwamba watu watatu wanashikiliwa na polisi wakihojiwa kufuatia tukio hilo.
==> Hili ni tukio la kwanza  katika historia ya uhifadhi nchini mwetu kwa Majangili kumpiga  risasi na kumuua Rubani na kisha  kuangusha helikopta .
==>Kepten Roger alikuwa akienda kuongeza nguvu ya askari wa uhifadhi waliokuwa wakipambana na majangili hatari wilayani Meatu, Simiyu katika ranchi ya wanyamapori ya Mwiba.

0 comments:

Post a Comment