Usiku wa February 24 muendelezo wa mechi ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ilipigwa kama kawaida, usiku wa February 24 ilipigwa michezo, klabu ya Man City ilikuwa ugenini kucheza dhidi ya Dynamo Kyiv, wakati ambao klabu ya PSV Endhoven ilikuwa ikicheza dhidi ya Atletico Madrid.
Kwa upande wa mashabiki wa Ligi Kuu soka Uingereza walikuwa na shauku ya kutaka kuona mchezo kati ya Dynamo Kyiv dhidi ya Man City, kwa mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi Man City walifanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1, licha ya kuwa walikuwa ugenini.
Man City walianza kupata goli la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Sergio Aguero, dakika ya 40 David Silva akapachika goli la pili, kipindi cha pili Dynamo Kyiv walirudi na kuanza kuonesha matumaini ya kutaka kusawazisha goli hizo, baada ya Vitaly Buyalsky kupachika goli la kwanza kwa Dynamo Kyiv dakika ya 58, Yaya Toure ndio aliwakatisha tamaa ya kuwezo kupata hata sare baada ya kupachika goli la tatu dakika ya 90.
Video ya magoli ya Dynamo Kyiv Vs Man City
0 comments:
Post a Comment