NI Muigizaji mkongwe wa hapa Bongo YETU, Mzee Jengua amesema kuwa ameshirikishwa katika filamu ya Sio Dili inayohusu mauaji ya Albino kutokana na hulka yake ya ukatili awapo kazini.
Akizungumza na Gazeti la Nipashe , Jengua alisema muandaaji wa filamu hiyo aliona yeye ndio anafaa kuwa mtu anayefanya biashara ya viungo vya Albino kutokana na uigizaji wake wa ukatili, katika filamu zilizopita.
Jengua hata hivyo amesema anaumizwa na tabia za watu ambao hukata viungo vya au kuwaua kwa imani za kishirikina .
“Filamu ya Sio Dili ni harakati ya kupambana na mauaji ya Albina na itakuwa elimu kwa watanzania wote alisema Jengua.
0 comments:
Post a Comment