+10 344 123 64 77

Sunday, May 24, 2015

BAADA YA KUWA MSHIDI MUIGIZAJI WA KIKE!!! IRENE PAUL ANA HAYA YA KUSEMA===>> endelea

Baada ya Kutajwa Kama Muigizaji Bora wa Kike Kwenye Tuzo Za TAFA 2015, Irene Paul Ameyasema Haya

     NI Staa NA  mrembo wa Bongo Movies, Irene Paul  ameibuka mshindi wa tuzo za Tanzania Film Awards  (TAFA) 2015 kwenye kipengele cha muigizaji bora wa kike ‘Best Actress (in Lead Role)’ ambapo alikuwa akichuana na Irene Veda ,Yvonne Cherrie ‘Monalisa’ , Rose Ndauka na Shamsa Ford.
    Irene  ameeleza kuwa  filamu ya Never Give Up aliyoicheza na staa kutoka Ghana  Van Vicker ndioiliyomfanya ashind tuzo hiyo.
    “Filamu iliyonifanya niwe msanii bora wa 2015 ni NEVER GIVE UP niliyoitwa na mzee kambi na niliyocheza na van vicker kutoka ghana van vicker” Ire alieleza  na kuongeza haya kupitia ukurasa wake mtandaoni
    “Yaani ni Laiti njia za Mungu zingekuwa za binadamu nahisi basi tungekuwa na historia tofauti,nasema hivyo maana natafakari nashindwa ila kwa vile amedhihirisha yupo na hana upendeleo NA AKISEMA NDIO HAKUNA WA KUPINGA,naongea na wewe kijana mwenye hitaji lako unaloamini ukifanikiwa utafika mahali fulani,haijalishi ni mda gani,haijalishi machoni pa wengi ni pagumu kiasi gani kinachojalisha ni nguvu na bidii unayoiweka katika kuitimiza ndoto yako ndipo patakapomfanya Mungu abariki na kuweka wepesi wa kupata ndoto yako THIS WAS MY DREAM" 
    Hongera sana Irene.

    0 comments:

    Post a Comment