Staa wa Bongo Movies, Rose Ndauka ambaye miaka miwili iliyopita alianzisha kipindi chake cha TV kilichopewa jina la ‘Family Talk Show’. Kupitia kampuni yake, muigizaji huyo alianza kurekodi episodes kadhaa za show hiyo ili zianze kuruka kwenye TV.
Hata hivyo kipindi hicho hakijawahi kuonekana na ni kama kiliishia hewani. “Kipindi changu.. niliibiwa vitu vyote ofisini lakini ndoto yangu ya utangazaji iko pale pale,” Hivi majuzi Rose aliiambia Kabali ya EFM.
Mwanzoni mwa mwaka 2013, Rose Ndauka alianza kushoot kipindi chake cha TV ambacho hata hivyo kiliishia hewani
March 23, 2013 kupitia akaunti yake ya Facebook, Rose aliweka picha akiwa studio akirekodi kipindi hicho na kuandika: MWAKA HALOOO TZ WELCOME TO THE FAMILY TALK SHOW FROM KIKOI TANZANIA LIMITED AND THAT IS OUR HOST=========>>> ROSE DONATUS NDAUKA, GET READY TO SEE NEW ROSE NDAUKA.”
0 comments:
Post a Comment