+10 344 123 64 77

Tuesday, May 19, 2015

BAADA YA LILE OVYO LA BASATA::: SHISHI BABY AFUNGUKA HAYA====>>soma zaidi

Baada ya Kupewa Onyo na BASATA, Shilole Afunguka


    NI Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ameeleza kusikitishwa na kitendo cha yule aliempiga picha zile akiwa stejini akitumbuiza  kwani ilikuwa ni bahati mbaya na sio makusudi.
    Shilole amesema kuwa hata yeye hakupenda kile kilichotokea jukwaani wakati akitumbuiza Ubelgiji hivi karibuni, kwa sababu ilikuwa bahati mbaya na hakudhamiria kukaa uchi kama wengi wanavyosema.
    Shishi ambaye ni mama wa watoto wawili amesema kuwa nguo mpya aliyoivaa siku hiyo ndio ilimponza kwasababu hakuwa ameifanyia majaribio ya kutumbuiza akiwa ameivaa.
    “Kiukweli kwasababu hili jambo limetokea inatakiwa nguo ninapoinunua niwe naifanyia training kwanza kabla ya kwenda jukwaani, kwahiyo kwasababu ile nguo ilikuwa mpya kwangu na sikuweza kuijua vizuri  yaani hii nguo nimeikuta huku huku, nguo imekuja kunitokea bahati mbaya wakati niko kwenye performAnce, ilitatuka wakati niko kwenye motion .” Alisema Shishi kupitia 255 ya Clouds Fm TZ.
    “Nasisitiza tena sikudhamiria na wala sikupenda hiyo kitu itokee, ila nasikitika kwamba kama mimi mwanamke yule mtu aliyenipiga picha na kudhamiria kuziweka kwenye mitandao alikuwa na maana gani, hakufikiria mimi nitaunmia kiasi gani au mashabiki wangu wataumia kiasi gani? Ni mtu mbaya mwenye roho mbaya sijui nimuiteje huyo mtu aliyefanya hivyo, sio mtu mzuri.”
    Kauli hii ya shilole ameitoa mara baada ya hivi karibuni Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kumpa onyo kali staa huyu kwa kitendo kilichotokea.
    Kuhusu kama amepokea barua ya kuitwa kujieleza kutoka BASATA, Shishi amesema kuwa hajapokea barua hiyo kwasababu bado yuko Ubelgiji.

    0 comments:

    Post a Comment