+10 344 123 64 77

Friday, June 5, 2015

BONGO MOVE!!! RAY>>> NASHANGAA SANA WANAOSEMA KANUMBA KAONDOKA NA TASNIA YA FILAM!!!!! SOMA ZAIDI HAPA MAELEZO YAKE

Ray Awashangaa Wanaodai Kanumba Ameondoka na Tasnia ya Filamu


     
    NI Staa mkubwa wa Bongo Movies, Vicent Kigosi >Ra< hivi juzi kati kupitia kukursa wake kwenye mtando picha wa Instagram amendika mtazamo juu ya tasnia ya filamu na wadau wote kwa ujumla.
    Napenda kuchukua furrsa hii kuwashukuru wadau wote kwa michango na sapoti yenu iliyosaidia kuifikisha tasnia ya filamu hapa ilipo.
    Bila nyinyi pengine hadithi ingekuwa tofauti leo kikubwa ni kujenga moyo wa kizalendo kwa wasanii wetu leo kuna misemo kila kona eti Kanumba kafa na tasnia imekufa, najaribu kuwaza kwa sauti hivi Kanumba si ndio huyu alikuwa anaambiwa hana jipya zaidi ya kupaka wave? Na si huyu huyu alipoingia katika jumba la Big Brother aliambiwa hajui kiingereza? Kuna watu wakamzomea na kumwita bogus, sasa leo baada ya kutangulia mbele ya haki amekuwa shujaa na kila kona anasifiwa.
    Watanzania tuwe wazalendo, mwenye sifa yake mpe akiwa hai umtie moyo kufanya kazi yake zaidi, sio ungojee akifa ndio uanze kumimina sifa.
    Mfano leo hii Diamond platinumz ni msanii anayefanya vizuri katika muziki pengine kuliko yeyote, ila kuna watu bila ya sababu za maana wanampinga na kusambaza chuki juu yake, hii inavunja moyo, tuweni wazalendo mpeni sifa zake angali hai, sio msubiri akishatangulia mbele ya haki muanze kusema kaenda na muziki wa bongo fleva....
    Maana yangu ni hii neema hujulikana ikishatoweka, hata hawa mnaowaona leo hawana maana wakishatangulia mbele ya haki watakuwa na thamani mno...huu ni mtazamo wangu tu- Ray alimaliza.

    0 comments:

    Post a Comment