Ilikuwa Story kubwa sana TZ mitandaoni na Magazetini, watu wakaikomalia ishu ya Umri, Elimu, na mengine mengi yanayomhusu aliyekuwa Miss TZ, Sitti Mtemvu.. mwisho wa yote akaamua kuvua Taji hilo ili kupisha kila kitu kilichokuwa kinaendelea.
Leo iko kwenye headlines tena kwenye masuala ya Urembo, Emily Kachote alikuwa Mrembo aliyeshinda Taji la Miss Zimbabwe 2015.. kingine kuhusu yeye leo kinahusu ishu ya Mrembo huyo kuvuliwa Taji baada ya kuzagaa kwa picha mbaya mitandaoni zikionesha akiwa mtupu.
Hii ishu ni kama wapo watakaoipokea vizuri, story za mitandaoni ni kwamba kumbe kuna baadhi ya watu hata hawakufurahia ushindi wa Emily aliposhinda Miss Zimbabwe na kuvalishwa Taji hilo.. walidai hakustahili ushindi huo.
0 comments:
Post a Comment