NI Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva, Hemmed Suleiman ‘Hemedy PHD’ambaye hivi karibuni atatamba mtaani na filamu ya FB Profile ameweka waz juu ya kukerwa na namna ushabiki wa sanaa nchini unavyopelekwa kwenye uadui na sio ushindani kam ilivyokuwa miaka michache iliyopita.
>>>Kiukweli kwenye sanaa tumeanza kwenda kwenye njia mbaya sana,aina hii ya ushabiki wa mtindo wa uadui itatupeleka pabaya sana..Mashabiki wa Ali Kiba , Wema sepetu na Diamond wanapaswa kuliona mapema tatizo hili,” alisema mkali huyo wa filamu ya Facebook.
Aidha , Hemmed amewaomba mashabiki wake kujiandaa kuipokea filamu yake mpya ya facebook Profile ambapo ndani ya filamu hiyo amaeigiza na wasanii Meya Shabani,Thadeo, Neema na wengineo, <<<Ni filamu nzuri sana itakayowavunja mbavu na kuwafundisha naomba muinunue itakapotoka”.
0 comments:
Post a Comment